THE DIVINE LITURGY OF PRESANCTIFIED GIFTS
ENARXIS
SHEMASI
DEACON
Ee padri, himidi.
Master, give the blessing.
KASISI
PRIEST
Mhimidiwa ni Ufalme wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.
Blessed is the kingdom of the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages.
WATU
CHOIR
Amina.
Amen.
INTRODUCTORY PSALM – PRAYERS
The Priest, during the reading of the Introductory Psalm, stands reverently before the altar table and reads the last three Vesperal Prayers, i.e. Prayers 5, 6, and 7. (Find these below after the Psalm.)
MSOMAJI
READER
Amina.
Amen.
Njooni, tumwinamie na tumsujudu Mungu mfalme wetu.
Come, let us worship and bow down before God our King.
Njooni, tumwinamie na tumsujudu Kristo yu Mungu mfalme wetu.
Come, let us worship and bow down before Christ God our King.
Njooni, tumwinamie na tumsujudu yeye, Kristo aliye mfalme na Mungu wetu.
Come, let us worship and bow down before Him, Christ our King and God.
Zaburi ya 103 (104).
Psalm 103 (104).
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Wewe, Bwana, Mungu wangu, umejifanya mkuu sana; umejivika heshima na adhama. Umejivika nuru kama vazi; umezitandika mbingu kama pazia; na kuziweka nguzo za orofa zake majini. Huyafanya mawingu kuwa gari lake, na kwenda juu ya mabawa ya upepo, huwafanya malaika zake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa moto wa miali. Uliiweka nchi juu ya misingi yake, isitikisike milele. Uliifunika kwa vilindi kama kwa vazi, maji yalikuwa yakisimama juu ya milima. Kwa kukemea kwako yakakimbia, kwa sauti ya radi yako yakaenda zake kasi, yakapanda milima, yakatelemka mabondeni, mpaka mahali ulipoyatengeneza. Umeweka mpaka yasiupite, wala yasirudi kuifunikiza nchi. Hupeleka chemchemi katika mabonde; zapita kati ya milima; zamnywesha kila mnyama wa kondeni; punda mwitu huzima kiu yao. Kandokando hukaa ndege wa angani; kati ya matawi hutoa sauti zao. Huinywesha milima toka orofa zake; nchi imeshiba mazao ya kazi zako. Huyameesha majani kwa makundi, na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; ili atoe chakula katika nchi, na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung''aze uso wake kwa mafuta, na mkate umburudishe mtu moyo wake. Miti ya Bwana nayo imeshiba, mierezi ya Lebanoni aliyoipanda. Ndimo ndege wafanyamo vitundu vyao, na korongo, misunobari ni nyumba yake. Milima mirefu ndiko waliko mbuzi wa mwitu, na magenge ni kimbilio la wibari. Aliufanya mwezi kwa ajili ya nyakati, jua latambua kuchwa kwake. Wewe hufanya giza, kukawa usiku, ndipo atambaapo kila mnyama wa mwitu. Wana-simba hunguruma wakitaka mawindo, ili kutafuta chakula chao kwa Mungu. Jua lachomoza, wanakwenda zao, na kujilaza mapangoni mwao. Mwanadamu atoka kwenda zake kazini, na kwenye utumishi wake mpaka jioni. Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako. Bahari iko kule, kubwa na upana, ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, viumbe hai vidogo kwa vikubwa. Ndimo zipitamo merikebu, ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, wao wanashiba mema; Wewe wauficha uso wako, wao wanafadhaika; waiondoa pumzi yao, wanakufa, na kuyarudia mavumbi yao. Waipeleka roho yako, wanaumbwa, nawe waufanya upya uso wa nchi. Utukufu wa Bwana na udumu milele; Bwana na ayafurahie matendo yake. Aitazama nchi, inatetemeka; aigusa milima, inatoka moshi. Nitamwimbia Bwana maadamu ninaishi; nitamshangilia Mungu wangu nikiwa hai; kutafakari kwangu na kuwe kutamu kwake; mimi nitamfurahia Bwana. Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Bless the Lord, O my soul. O Lord my God, You are magnified exceedingly; You clothe Yourself with thanksgiving and majesty, who cover Yourself with light as with a garment, who stretch out the heavens like a curtain; You are He who covers His upper chambers with water, who makes the clouds His means of approach, who walks on the wings of the winds, who makes His angels spirits and His ministers a flame of fire. He established the earth on its stable foundation; it shall not be moved unto ages of ages. The deep like a garment is His covering; the waters shall stand upon the mountains; at Your rebuke they shall flee; at the sound of Your thunder, they shall be afraid. The mountains rise up, and the plains sink down to the place You founded for them. You set a boundary they shall not pass over; neither shall they return to cover the earth. You are He who sends springs into the valley; the waters shall pass between the mountains; they shall give drink to all the wild animals of the field; the wild asses shall quench their thirst; the birds of heaven shall dwell beside them; they shall sing from the midst of the rocks. You are He who waters the mountains from His higher places; the earth shall be satisfied with the fruit of Your works. You are He who causes grass to grow for the cattle, and the green plant for the service of man, to bring forth bread from the earth; and wine gladdens the heart of man, to brighten his face with oil; and bread strengthens man’s heart. The trees of the plain shall be full of fruit, the cedars of Lebanon, which You planted; there the sparrows shall make their nests; the house of the heron takes the lead among them. The high mountains are for the deer; the cliff is a refuge for the rabbits. He made the moon for seasons; the sun knows its setting. You established darkness, and it was night, wherein all the wild animals of the forest will prowl about; the young lions roar and snatch their prey, and seek their food from God. The sun arises, and they are gathered together; and they shall be put to bed in their dens. Man shall go out to his work and to his labor until evening. O Lord, Your works shall be magnified greatly; You made all things in wisdom; the earth was filled with Your creation. There is this great and spacious sea: the creeping things are there without number; the living things are there, both small and great; there the ships pass through; there is this dragon You formed to play therein. All things wait upon You, that You may give them food in due season. When You give it to them, they shall gather it; when You open Your hand, all things shall be filled with Your goodness. But when You turn Your face away, they shall be troubled; when You take away their breath, they shall die and return again to their dust. You shall send forth Your Spirit, and they shall be created, and You shall renew the face of the earth. Let the glory of the Lord be forever; the Lord shall be glad in His works; He looks upon the earth and makes it tremble; He touches the mountains, and they smoke. I will sing to the Lord all my life; I will sing to my God as long as I exist; may my words be pleasing to Him, and I shall be glad in the Lord. May sinners cease from the earth, and the lawless, so as to be no more. Bless the Lord, O my soul.
Jua latambua kuchwa kwake; Wewe hufanya giza kukawa usiku,
The sun knows its setting. You established darkness, and it was night.
Ee Bwana, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. [[SWA]]
O Lord, Your works shall be magnified greatly; You made all things in wisdom. [SAAS]
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Glory to the Father and the Son and the Holy Spirit. Both now and ever and to the ages of ages. Amen.
Alleluia, Alleluia, a|leluia. Utukufu kwako, Ee Mungu. (3)
Alleluia. Alleluia. Alleluia. Glory to You, O God. (3)
Matumaini yetu, Ee Bwana, utukufu kwako.
Our hope, O Lord, glory to You.
SHEMASI
DEACON
Kwa amani, tumwombe Bwana.
In peace let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya amani kutoka juu na ya wokovu wa roho zetu, tumwombe Bwana.
For the peace from above and for the salvation of our souls, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya amani ya dunia yote, na kusimama imara kwa Ekklesia Takatifu ya Mungu, na ya umoja wa wote, tumwombe Bwana.
For the peace of the whole world, for the stability of the holy churches of God, and for the unity of all, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya nyumba hii takatifu na waingiamo kwa imani, heshima na kumcha Mungu, tumwombe Bwana.
For this holy house and for those who enter it with faith, reverence, and the fear of God, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya wakristo wateule na waorthodoksi wote, tumwombe Bwana.
For pious and Orthodox Christians, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya Askofu wetu mkuu Askofu wetu mkuu (jina) Makasisi, Mashemasi wateule na watu wote tumwombe Bwana.
For our Archbishop (name), for the honorable presbyterate, for the diaconate in Christ, and for all the clergy and the people, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya taifa letu (jina) na raisi wetu (jina), na viongozi wetu, na wa majeshi wapendao dini, tumwombe Bwana.
For our country, the president, all those in public service, and for our armed forces everywhere, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya mji huu na miji yote na nchi zote na waishimo kwa imani, tumwombe Bwana.
For the Holy and Great Church of Christ, for our Sacred Archdiocese, [for this Sacred Metropolis,] for this city and parish, for every city and land, and for the faithful who live in them, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya majira mema ya mwaka kupata mvua ya kutosha na hewa safi na rotuba ya kutosha kwa ardhi, tumwombe Bwana.
For favorable weather, for an abundance of the fruits of the earth, and for peaceful times, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya wasafiri hewani juu, baharini majini, na nchini kavu, wachoshwa na mateka kupata uhuru, na kwa ajili ya wokovu wao, tumwombe Bwana.
For those who travel by land, sea, and air, for the sick, the suffering, the captives and for their salvation, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sitikiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.
For our deliverance from all affliction, wrath, danger, and distress, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.
Remembering our all-holy, immaculate, most blessed, and glorious Lady, the Theotokos and ever-virgin Mary, with all the saints, let us commend ourselves and one another and our whole life to Christ our God.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
VESPERAL PRAYER 1
Tumwombe Bwana, Bwana hurumiaEe Bwana, mvumilivu, mwenye huruma nyingi na mpenda wanadamu yasikie sala zetu na utege sikio lako kwa sauti ya maombi yetu. Imarisha agano jema kwetu; ma utuongoze tuishi kwa ukweli wako. Furahisha mioyo yetu tulitii jina lako takatifu; u mkubwa na mtenda maajabu, Mungu wa pekee na hakuna mungu mwingine kama Wewe, Ee Bwana; wa fadhili na wa uwezo unayetusaidia, kutegemeza na kuwaokoa wanaotumaini jina lako takatifu. Kwa kuwa utukufu, heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwanaa na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milelel na milelel. Amina..
Lord, compassionate and merciful, longsuffering and abounding in mercy, give ear to our prayer and heed the voice of our supplication. Work a sign in our midst for good. Lead us in Your way, and we will walk in Your truth; gladden our hearts so as to fear Your holy name. For You are great and You do wonders; You alone are God, and there is none like You among the gods. Lord, You are mighty in mercy and good in strength, to help and comfort and save all those who hope in Your holy name.
KASISI
PRIEST
Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele. ( Amina. )
For to You belong all glory, honor, and worship, to the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages. ( Amen. )
MSOMAJI
READER
First Stanza.
Zaburi ya 119 (120).
Psalm 119 (120).
Katika shida yangu nalimlilia BWANA naye akaniitikia. Ee BWANA, uiponye nafsi yangu na midomo ya uongo na ulimi wa hila. Akupe nini, akuzidishie nini, ewe ulimi wenye hila? Mishale ya mtu hodari iliyochongoka, pamoja na makaa ya mretemu. Ole wangu mimi! Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki; na kufanya maskani yangu katikati ya hema za Kedari. Nafsi yangu imekaa siku nyingi, pamoja naye aichukiaye amani. Mimi ni wa amani; bali ninenapo, wao huelekea vita. [[SWA]]
To the Lord in my affliction I cried out, and He heard me. O Lord, deliver my soul from unjust lips and from a deceitful tongue. What should be given You, and what added to You, against a deceitful tongue? The arrows of the Mighty One are sharpened with hot coals from the desert. Woe is me! My sojourning was prolonged; I dwelt with the tents of Kedar. My soul sojourned a long time as a resident alien. With those who hate peace, I was peaceful; when I spoke to them, they made war against me without cause. [SAAS]
Zaburi ya 120 (121).
Psalm 120 (121).
Nitayainua macho yangu niitazame milima, msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika BWANA, aliyezifanya mbingu na nchi. Asiuache mguu wako usogezwe; asisinzie akulindaye; naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli. BWANA ndiye mlinzi wako; BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana, wala mwezi wakati wa usiku. BWANA atakulinda na mabaya yote, atakulinda nafsi yako. BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, tangu sasa na hata milele. [[SWA]]
I lifted my eyes to the mountains; from where shall my help come? My help comes from the Lord, who made heaven and earth. Let not your foot be moved; neither let Him who keeps you slumber. Behold, He who keeps Israel shall neither slumber nor sleep. The Lord shall keep you; the Lord is your shelter at your right hand. The sun shall not burn you by day nor the moon by night. The Lord shall keep you from all evil; the Lord shall keep your soul. The Lord shall keep your coming in and your going out from this present time and unto the ages. [SAAS]
Zaburi ya 121 (122).
Psalm 121 (122).
Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa BWANA. Miguu yetu imesimama ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu. Ee Yerusalemu uliyejengwa kama mji ulioshikamana, huko ndiko walikopanda kabila, kabila za BWANA; ushuhuda kwa Israeli, walishukuru jina la BWANA. Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya mbari ya Daudi. Utakieni Yerusalemu amani; na wafanikiwe wakupendao; amani na ikae ndani ya kuta zako, na kufanikiwa ndani ya majumba yako. Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu niseme sasa, Amani ikae nawe. Kwa ajili ya nyumba ya BWANA, Mungu wetu, nikutafutie mema. [[SWA]]
I was glad when they said to me, “Let us go into the house of the Lord.” Our feet stand in your courts, O Jerusalem. Jerusalem is built as a city whose compactness is complete. There the tribes went up, the tribes of the Lord, a testimony to Israel, to give thanks to the name of the Lord. For thrones sat there for judgment, thrones over the house of David. Ask now for things regarding the peace of Jerusalem, and there is prosperity for those who love you; let there now be peace in your power and prosperity in your citadels. For the sake of my brothers and my neighbors, I indeed spoke peace concerning you; for the sake of the house of the Lord our God, I sought good things for you. [SAAS]
Zaburi ya 122 (123).
Psalm 122 (123).
Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni. Kama vile macho ya watumishi kwa mkono wa bwana zao, kama macho ya mjakazi kwa mkono wa bibi yake; hivyo macho yetu humwelekea BWANA, Mungu wetu, hata atakapoturehemu. Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu sisi, kwa maana tumeshiba dharau. Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, na dharau ya wenye kiburi. [[SWA]]
I lift my eyes to You, who dwell in heaven. Behold, as the eyes of servants look to the hands of their masters, as the eyes of the maidservant look to the hands of her mistress, so our eyes look to the Lord our God until He shall have compassion on us. Have mercy on us, O Lord, have mercy on us, for we are greatly filled with contempt; our soul is greatly filled with it. We are a disgrace to those who prosper, and a contempt to the arrogant. [SAAS]
Zaburi ya 123 (124).
Psalm 123 (124).
Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, Israeli na aseme sasa, Kama si BWANA aliyekuwa pamoja nasi, wanadamu walipotushambulia, papo hapo wangalitumeza hai, hasira yao ilipowaka juu yetu. Papo hapo maji yangalitugharikisha, mto ungalipita juu ya roho zetu; papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu maji yafurikayo. Na ahimidiwe BWANA; asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. Nafsi yetu imeokoka kama ndege katika mtego wa wawindaji, mtego umevunjika, nasi tumeokoka. Msaada wetu u katika jina la BWANA, aliyezifanya mbingu na nchi. [[SWA]]
“If the Lord had not been with us,” let Israel now say, “If the Lord had not been with us, when men rose up against us, then they would have swallowed us alive, when their anger raged against us, then the water would have drowned us; our soul would have passed through a torrent, then our soul would have passed through a water that is overwhelming.” Blessed is the Lord, who did not give us as prey to their teeth. Our soul was delivered like a sparrow from the snare of the hunters; the snare was broken, and we were delivered. Our help is in the name of the Lord, who made heaven and earth. [SAAS]
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Glory to the Father and the Son and the Holy Spirit. Both now and ever and to the ages of ages. Amen.
Alleluia, Alleluia, a|leluia. Utukufu kwako, Ee Mungu. (3)
Alleluia. Alleluia. Alleluia. Glory to You, O God. (3)
Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.
Lord, have mercy. Lord, have mercy. Lord, have mercy.
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Glory to the Father and the Son and the Holy Spirit. Both now and ever and to the ages of ages. Amen.
SHEMASI
DEACON
Tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.
Again and again in peace let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.
Remembering our all-holy, immaculate, most blessed, and glorious Lady, the Theotokos and ever-virgin Mary, with all the saints, let us commend ourselves and one another and our whole life to Christ our God.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
Ombi la Antifono ya Pili
VESPERAL PRAYER 2
Tumwombe Bwana, Bwana hurumia Ee Bwana usitukemee na kutuadhibu kwa hasira yako, bali utupe kwa kadiri ya upole wako uliye mganga na mponyaji wa Roho zetu. UTuongoze kwenye kimbilio la nia yako na kuangaza mioyo yetu kujua ukweli walo. Tena, utujalie usiku huu na siku zote za maisha yetu ziwe za amani, bila dhambi, kwa maombi ya mzazi Mungu mtakatifu na ya watakatifu wote. Kwa kuwa utawala ni wako na ufalme na nguvu na utukufu ni vyako, vya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.
O Lord, do not rebuke us in Your wrath, nor chasten us in Your anger. But deal with us according to Your kindness, O physician and healer of our souls. Guide us to the haven of Your desire. Enlighten the eyes of our hearts to the knowledge of Your truth. And grant us to pass the rest of the day, and the entire time of our life, in peace and without sin; at the intercessions of the holy Theotokos and all Your saints.
KASISI
PRIEST
Kwa kuwa, utawala ni kwako na ufalme na uweza, na utukufu ni vyako, Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele. ( Amina. )
For Yours is the dominion, and Yours is the kingdom and the power and the glory, of the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages. ( Amen. )
MSOMAJI
READER
Second Stanza.
Zaburi ya 124 (125).
Psalm 124 (125).
Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, tangu sasa na hata milele. Kwa maana fimbo ya udhalimu haitakaa juu ya fungu la wenye haki; wenye haki wasije wakainyosha mikono yao kwenye upotovu. Ee BWANA, uwatendee mema walio wema, nao walio wanyofu wa moyo. Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka, BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani ikae na Israeli. [[SWA]]
Those who trust in the Lord are like Mount Zion; he who dwells in Jerusalem shall be unshaken forever. The mountains surround her, and the Lord surrounds His people from this present time and unto the ages. The Lord will not permit the rod of sinners to be upon the inheritance of the righteous, lest the righteous stretch out their hands in lawlessness. Do good, O Lord, to the good, and to the upright in heart; but those who turn aside to crooked ways, the Lord shall lead away with the workers of lawlessness. Peace be upon Israel. [SAAS]
Zaburi ya 125 (126).
Psalm 125 (126).
BWANA alipowarejeza mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto. Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, BWANA amewatendea mambo makuu. BWANA alitutendea mambo makuu, tulikuwa tukifurahi. Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa, kama vijito vya Kusini. Wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, azichukuapo mbegu za kupanda, hakika atarudi kwa kelele za furaha, aichukuapo miganda yake. [[SWA]]
When the Lord returned the captives of Zion, we became like those who are comforted. Then our mouth was filled with joy, and our tongue with exceeding joy. Then they shall say among the Gentiles, “The Lord did great things with them.” The Lord has done great things with us; we were glad. Return, O Lord, our captivity like streams in the south. Those who sow with tears shall reap with exceeding joy. They went forth and wept, carrying their seeds with them; but they shall return with exceeding joy, carrying their sheaves. [SAAS]
Zaburi ya 126 (127).
Psalm 126 (127).
BWANA asipoijenga nyumba waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure. Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, na kukawia kwenda kulala, na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi. Tazama, wana ndio urithi wa BWANA, uzao wa tumbo ni thawabu. Kama mishale mkononi mwa shujaa, ndivyo walivyo wana wa ujanani. Heri mtu yule aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu wanaposema na adui langoni. [[SWA]]
Unless the Lord builds the house, those who build it labor in vain; unless the Lord guards the city, those who guard it stay awake in vain. It is in vain for you to rise early, to awaken from your rest, you who eat the bread of grief, when He gives His beloved ones sleep. Behold, children are the Lord’s inheritance; the fruit of the womb His reward. Like arrows in the hand of a mighty one, so are the children of those who were outcasts. Blessed is the man who shall fulfill his desire with them; they shall not be ashamed, when they speak to their enemies at the gate. [SAAS]
Zaburi ya 127 (128).
Psalm 127 (128).
Heri kila mtu amchaye BWANA, aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; utakuwa heri, na kwako kwema. Mkeo atakua kama mzabibu uzaao, vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizetuini wakizunguka meza yako. Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA. BWANA akubariki toka Sayuni; uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli. [[SWA]]
Blessed are all who fear the Lord, who walk in His ways. You shall eat the fruits of your labor; you are blessed, and it shall be well with you. Your wife shall be like a vine, prospering on the sides of your house; your children like newly planted olive trees around your table. Behold, so shall the man be blessed who fears the Lord. May the Lord bless you from Zion, and may you see the good things of Jerusalem all the days of your life; may you see your children’s children. Peace be upon Israel. [SAAS]
Zaburi ya 128 (129).
Psalm 128 (129).
Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa, Mara nyingi wamenitesa tangu ugana wangu, lakini hawakuniweza. Wakulima wamelima mgongoni mwangu, wamefanya mirefu mifuo yao. BWANA ndiye mwenye haki, amezikata kamba zao wasio haki. Na waaibishwe, warudishwe nyuma, wote wanoichukia Sayuni. Na wawe kama majani ya darini yanyaukayo kabla hayajamea. Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, wala mfunga miganda kifua chake. Wala hawasemi wapitao, Amani ya BWANA ikae nanyi, twawabariki kwa jina la BWANA. [[SWA]]
“Many times they warred against me from my youth,” let Israel now say; “Many times they warred against me from my youth, yet they did not overcome me. The sinners schemed behind my back; they prolonged their lawlessness.” The righteous Lord cut in pieces the necks of sinners. Let all who hate Zion be shamed and turned back. Let them become like grass on the housetops, which withers before it is plucked up; like grass with which the reaper does not fill his hand, nor the gatherer of sheaves, his bosom; neither do those who pass by say to them, “The Lord’s blessing be upon you; in the Lord’s name, we bless you.” [SAAS]
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Glory to the Father and the Son and the Holy Spirit. Both now and ever and to the ages of ages. Amen.
Alleluia, Alleluia, a|leluia. Utukufu kwako, Ee Mungu. (3)
Alleluia. Alleluia. Alleluia. Glory to You, O God. (3)
Bwana hurumia, Bwana hurumia, Bwana hurumia.
Lord, have mercy. Lord, have mercy. Lord, have mercy.
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Glory to the Father and the Son and the Holy Spirit. Both now and ever and to the ages of ages. Amen.
SHEMASI
DEACON
Tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.
Again and again in peace let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.
Remembering our all-holy, immaculate, most blessed, and glorious Lady, the Theotokos and ever-virgin Mary, with all the saints, let us commend ourselves and one another and our whole life to Christ our God.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI LA ANTIFONO YA TATU
VESPERAL PRAYER 3
Ee Bwana Mungu wetu, utukumbuke sisi watumishi wako wenye dhambi wasiofaa tutajapo jina lako takatifu na tuwekapo tumaini letu kwa rehema yako, bali utujalie kwa yale yote tunayokuomba kwa ajili ya wokovu wetu, Ee Bwana; utufanye wafaao kukupenda na kukuogopa kwa mioyo yetu yote na kumarisha nia yako kwa vitu vyote. Kwa kuwa u Mwenye rhema na mpenda wanadamu na kwako tunatoa utukufu kwa Baba na MWana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Lord our God, remember us Your sinful and unworthy servants when we call upon Your holy name; and do not put us to shame as we anticipate Your mercy. Please, Lord, grant us all our requests that lead to salvation; and grant that we may wholeheartedly love and fear You and do Your will in all things.
KASISI
PRIEST
Kwa kuwa U Mungu Mwema na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa Utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele. ( Amina. )
For You are good and benevolent God, and to You we offer up glory, to the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages. ( Amen. )
MSOMAJI
READER
Third Stanza.
Zaburi ya 129 (130).
Psalm 129 (130).
Ee BWANA, toka vilindini nimekulilia. Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize sauti ya dua zangu. BWANA, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, ili Wewe uogopwe. Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja, na neno lake nimelitumainia. Nafsi yangu inamngoja Bwana, kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, naam, walinzi waingojao asubuhi. Ee Israeli, umtarajie BWANA; maana kwa BWANA kuna fadhili, na kwake kuna ukombozi mwingi. Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote. [[SWA]]
Out of the depths I have cried to You, O Lord; O Lord, hear my voice; let Your ears be attentive to the voice of my supplication. If You, O Lord, should mark transgression, O Lord, who would stand? For there is forgiveness with You. Because of Your law, O Lord, I waited for You; my soul waited for Your word. My soul hopes in the Lord, from the morning watch until night; from the morning watch until night, let Israel hope in the Lord. For with the Lord there is mercy, and with Him is abundant redemption; and He shall redeem Israel from all his transgressions. [SAAS]
Zaburi ya 130 (131).
Psalm 130 (131).
BWANA, moyo wangu hauna kiburi, wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, wala na mambo yashindayo nguvu zangu. Hakika nimeituliza nafsi yangu, na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa kifuani mwa mama yake; kama mtoto aliyeachishwa, ndivyo roho yangu ilivyo kwangu. Ee Israeli, umtarajie BWANA, tangu leo na hata milele. [[SWA]]
O Lord, my heart is not exalted, neither are my eyes raised up; neither am I carried along in great things, nor in things too marvelous for me. If I were not humble-minded, but exalted my soul, like a child weaned from his mother, so You would reward my soul. Let Israel hope in the Lord from this present time and unto the ages. [SAAS]
Zaburi ya 131 (132).
Psalm 131 (132).
BWANA, umkumbukie Daudi taabu zake zote alizotaabika. Ndiye aliyemwapia BWANA, akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo. Sitaingia hemani mwa nyumba yangu, wala sitapanda matandiko ya kitanda changu; sitaacha macho yangu kuwa na usingizi, wala kope zangu kusinzia; hata nitakapompatia BWANA mahali, na Shujaa wa Yakobo maskani. Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata, katika konde la Yearimu tuliiona. Na tuingie katika maskani yake, tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake. Ee BWANA, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako. Makuhani wako na wavikwe haki, watauwa wako na washangilie. Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako, usiurudishe nyuma uso wa masihi wako. BWANA amemwapia Daudi neno la kweli, hatarudi nyuma akalihalifu, Baadhi ya wazao wa mwili wako nitawaweka katika kiti chako cha enzi. Wanao wakiyashika maagano yangu, na shuhuda nitakazowafundisha; watoto wao nao wataketi katika kiti chako cha enzi milele. Kwa kuwa BWANA ameichagua Sayuni, ameitamani akae ndani yake. Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele, hapo nitakaa kwa maana nimepatamani. Hakika nitavibariki vyakula vyake, wahitaji wake nitawashibisha chakula. Na makuhani wake nitawavika wokovu, na watauwa wake watashangilia. Hapo nitamchipushia Daudi pembe, na taa nimemtengenezea masihi wangu. Adui zake nitawavika aibu, bali juu yake taji yake itasitawi. [[SWA]]
Remember David, O Lord, and all his meekness, how he swore to the Lord, how he vowed to the God of Jacob, “I shall not enter my dwelling, I shall not recline on my bed, I shall not close my eyes in sleep nor my eyelids for dozing, nor give any rest to my temples, until I find a place for the Lord, a tabernacle for the God of Jacob.” Behold, we heard of it in Ephrathah; we found it in the plains of the wood; let us enter into His tabernacles; let us worship at the place where His feet stood. Arise, O Lord, into Your rest, You and the ark of Your holiness; Your priests shall clothe themselves in righteousness; Your saints shall greatly rejoice. For Your servant David’s sake, do not turn away from the face of Your anointed. The Lord swore to David this truth, and He shall not reject it, “I shall set upon your throne one from the fruit of your loins. If your sons keep My covenant and these testimonies I shall teach them, then their sons shall sit upon your throne forever.” For the Lord has chosen Zion; He chose her for His dwelling: “This is My place of rest unto ages of ages; here I shall dwell, for I have chosen her. Blessing, I shall bless her provision; I shall satisfy her poor with bread; and I shall clothe her priests with salvation, and her saints shall rejoice exceedingly with great joy; there I shall cause to spring up a horn for David; there I prepared a lamp for my anointed; his enemies I shall clothe with shame; upon him shall My sanctification flourish.” [SAAS]
Zaburi ya 132 (133).
Psalm 132 (133).
Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko BWANA alikoamuru baraka, naam, uzima hata milele. [[SWA]]
Behold now, what is so good or so pleasant as for brothers to dwell together in unity? It is like fragrant oil running down upon the beard, the beard of Aaron, running down upon the border of his garment; it is like the dew of Hermon, running down upon the mountains of Zion; for there the Lord commanded the blessing and life forever. [SAAS]
Zaburi ya 133 (134).
Psalm 133 (134).
Tazama, enyi watumishi wa BWANA, mhimidini BWANA, nyote pia. Ninyi mnaosimama usiku katika nyumba ya BWANA. Painulieni patakatifu mikono yenu, na kumhimidi BWANA. BWANA akubariki toka Sayuni, aliyezifanya mbingu na nchi. [[SWA]]
Behold now, bless the Lord, all you servants of the Lord, who stand in the house of the Lord, in the courts of the house of our God. In the nights, lift up your hands to the holy of holies and bless the Lord. May the Lord bless you from Zion, He who made heaven and earth. [SAAS]
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Glory to the Father and the Son and the Holy Spirit. Both now and ever and to the ages of ages. Amen.
Alleluia, Alleluia, a|leluia. Utukufu kwako, Ee Mungu. (3)
Alleluia. Alleluia. Alleluia. Glory to You, O God. (3)
Matumaini yetu, Ee Bwana, utukufu kwako.
Our hope, O Lord, glory to You.
SHEMASI
DEACON
Tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.
Again and again in peace let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Tumkumbuke Maria Mtakatifu kamili, asiye na doa, Mbarikiwa zaidi kushinda wote, Bibi wetu mtukufu mzazi Mungu na bikira daima pamoja na watakatifu wote hata sisi pia wenyewe na kila mmoja wetu na wenzetu wote, hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.
Remembering our all-holy, immaculate, most blessed, and glorious Lady, the Theotokos and ever-virgin Mary, with all the saints, let us commend ourselves and one another and our whole life to Christ our God.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI LA ANTIFONO YA NNE
VESPERAL PRAYER 4
Ewe, unayesifiwa kwa nguvu takatifu, kwa nyimbo za utukufu zisizo kuwa na mwisho, ujaze vinywa vyetu na utukufu wako ili tulihimidi jina lako takatifu; na utuunganishe na utupe urithi pamoja nao wakuogopao katika ukweli na wanaotunza amri zako; kwa maombi ya mtakatifu Mzazi Mungu na watakatifu wako, kwa kuwa wastahili wote, heshima na usjudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
O Lord, extolled by the holy hosts with never-silent hymns and never-ceasing doxologies, fill our mouths with Your praise, to ascribe greatness to Your holy name. Give us a portion and inheritance with all those who fear You in truth and keep Your commandments; at the intercessions of the holy Theotokos and all Your saints.
KASISI
PRIEST
( Amina. )
For You are our God, the God of mercy and salvation, and to You do we offer up glory, to the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages. ( Amen. )
SHEMASI
DEACON
(kwa mnong''ono)
(in a low voice)
Tumwombe Bwana.
Let us pray to the Lord.
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
Ombi la Kuingia.
ENTRANCE PRAYER
Jioni, asubuhi na adhuhuri twakusifu, twakuhimidi, twakushukuru na twakuomba, Ee Rabi wa wote, Bwana mpenda wanadamu. Elekeza maombi yetu mbele zako kama uvumba, na mioyo yetu isipotoshwe kwenye maneno namafikira maovu, utuokoe kwa kila jaribio rohoni mwetu; kwa kuwa macho yetu yaelekea kwako ewe Bwana na tumekukimbilia wewe, usituambishe, Ee Mungu wetu, (kwa sauti):Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, Baba na Mwana na Roho Mtaktifu, sasa na siku zote hata milele na milele.
In the evening, in the morning, and at midday, we praise You, we bless You, we give thanks to You, and we pray to You, Master of all, benevolent Lord. Let our prayer be set forth before You as incense. Incline not our hearts to evil words or thoughts, but deliver us all from those who pursue our souls. For our eyes, O Lord, O Lord, are toward You, and in You we hope. Leave us not embarrassed, O our God.
SHEMASI
DEACON
Hekima. Simameni wima.
Wisdom. Arise.
MSOMAJI
READER
We Nuru ya furaha ya utukufu mtakatifu, ya Baba usiyekufa, wa mbinguni, mtakatifu, mhimidiwa, Yesu Kristo! Tukiwa tumefika wakati wa kuchwa kwa jua na kuona mwanga wa jioni tunamwimbia Baba, Mwana na Roho Mtakatifu Mungu. Ni wajibu wakati wote usifiwe kwa sauti safi, Ee Mwana wa Mungu, mpaji wa uhai; kwa hivyo dunia ya kutukuza.
Gladsome light of holy glory of the holy, blessed, heavenly, immortal Father, O Jesus Christ: arriving at the hour of sunset and having seen the evening light, we praise the Father, Son, and Holy Spirit, God. It is worthy for You to be praised at all times with happy voices, O Son of God and Giver of life; * and therefore the world glorifies You.
SHEMASI
DEACON
Jioni...
The evening…
(sung)
Command!
KASISI
PRIEST
Hekima. Simameni wima.
Wisdom. Arise. The light of Christ elucidates everything.
MSOMAJI
READER
KASISI
PRIEST
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
Let my prayer be set forth before You as incense, the lifting up of my hands as the evening sacrifice.
Ee Bwana nimekuita, unijie hima, unijie hima, Bwana. Ee Bwana nimekuita, unijie hima, uisikie sauti ya kilio changu, uisikie sauti yangu nikuitapo.
Lord, I have cried to You; hear me. Hear me, O Lord. Lord, I have cried to You; hear me. Give heed to the voice of my supplication when I cry to You.
WATU
CHOIR
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
Let my prayer be set forth before You as incense, the lifting up of my hands as the evening sacrifice.
KASISI
PRIEST
Ee Bwana uweke mlinzi kinywani pangu na mngojezi midomo yangu.
Set a watch, O Lord, before my mouth, a door of enclosure about my lips.
WATU
CHOIR
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
Let my prayer be set forth before You as incense, the lifting up of my hands as the evening sacrifice.
KASISI
PRIEST
Usiulekeze moyo wangu kunako maneno mabaya, nisiyazoee matendo yasiyofaa.
Incline not my heart to evil words, to make excuses in sins.
WATU
CHOIR
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
Let my prayer be set forth before You as incense, the lifting up of my hands as the evening sacrifice.
KASISI
PRIEST
Utukufu kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. Sasa na siku zote hata milele na milele. Amina.
Glory to the Father and the Son and the Holy Spirit. Both now and ever and to the ages of ages. Amen.
WATU
CHOIR
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.
Let my prayer be set forth before You as incense, the lifting up of my hands as the evening sacrifice.
KASISI
PRIEST
Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba.
Let my prayer be set forth before You as incense.
WATU
CHOIR
Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni. [[SWA]]
The lifting up of my hands as the evening sacrifice. [SAAS]
SHEMASI
DEACON
Tuseme sisi sote kwa roho yetu na kwa mawazo yetu yote tuseme hivi.
Let us all say with all our soul and with all our mind, let us all say.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ee Bwana Mwenyezi Mungu wa mababu wetu tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.
Lord, Ruler of all, God of our fathers, we pray You, hear us and have mercy.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utuhurumie, Ee Mungu kadiri ya huruma yako kubwa, tunakuomba utusikilize na kutuhurumia.
Have mercy on us, O God, according to Your great mercy, we pray You, hear us and have mercy.
( Bwana, hurumia. (3) )
( Lord, have mercy. (3) )
Tena tunakuomba kwa ajili ya Wakristo watawa waorthodoksi wote.
Again we pray for pious and Orthodox Christians.
( Bwana, hurumia. (3) )
( Lord, have mercy. (3) )
Tena tunaomba kwa ajili ya Askofu wetu mkuu (jina)
Again we pray for our Archbishop (name).
( Bwana, hurumia. (3) )
( Lord, have mercy. (3) )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
Ee Bwana Mungu wetu, pokea maombi haya yenye moyo wa bidii ya watumwa wako, na utuhurumie kadiri ya wingi wa huruma zako; utupatie sisi Baraka zako na kwa watu wako wote wanaongoja huruma yako kubwa nay a utajiri.
Lord our God, accept this fervent supplication from Your servants, and have mercy on us in accordance with the abundance of Your mercy, and send down Your compassion upon us and upon all Your people who await Your great and rich mercy.
KASISI
PRIEST
Kwa kuwa U Mungu mrahimu na mpenda wanadamu, na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.
For You are merciful and benevolent God, and to You we offer up glory, to the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
SHEMASI
DEACON
Enyi wakatekumeno ombeni kwa Bwana.
Catechumens, pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Hata sisi tulioamini tuombe Bwana kwa ajili ya wakatekumeno.
Let us, the faithful, pray for the catechumens.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ili awahurumie.
That the Lord have mercy on them.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Awafahamishe neno la ukweli.
That He teach them the word of truth.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Awafunulie Evangelio ya haki.
That He reveal to them the gospel of righteousness.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Awaunganishe kwa Kanisa lake moja takatifu Katholiki na la kimitume.
That He unite them to His holy, catholic, and apostolic Church.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Uwaokoe, uwahurumie, uwahifadhi, uwalinde Ee Mungu kwa neema yako.
Save them, have mercy on them, help them, and protect them, O God, by Your grace.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Enyi wakatekumeno inamisheni vichwa vyenu kwa Bwana.
Catechumens, bow your heads to the Lord.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI LA WAKATEKUMENO
PRAYER FOR CATECHUMENS
Ewe Bwana na Mungu wetu, mwumba wa viumbe vyote, unayependa watu wote kuona wokovu na kupata kujua maarifa ya ukweli wako, waangalie watumwa wako wakatikumeno na uwaokoe na dhambi zao za asili na hila za uadui; waite uzimani kwa kuangazia nafsi na miili yao na uwahesabie pamoja na kundi lako la kweli ambalo kwalo jina lako takatifu hutajwa.
God, our God, creator and maker of all, as You will that everyone be saved and come to the knowledge of the truth, look upon your servants, the catechumens, and rescue them from the ancient error and from the devil''s devices. Invite them to eternal life; illumine their souls and bodies; and include them in Your rational flock, over which Your holy name has been invoked.
KASISI
PRIEST (aloud)
Ili hawa pia pamoja nasi walitukuze jina lako adhimu na linaloheshimiwa ajabu, la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.
So that with us they also may glorify Your most honorable and majestic name, of the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
SHEMASI
DEACON
Wakatikumeno tokeni, enyi wakatikumeno tokeni. Wakatekumeno wote, tokeni; mkatikumeno asibaki.
All catechumens, depart; catechumens depart. All catechumens, depart. Let no catechumen remain.
LITANIES FOR THE FAITHFUL
SHEMASI
DEACON
Walioamini, tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.
All the faithful, again and again in peace let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako. Hekima.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace. Wisdom.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI LA KWANZA LA WAUMINI
FIRST PRAYER FOR THE FAITHFUL
Ee Mungu mkuu na unayesifiwa, uliyetuleta kwenye ukamilifu kutika uharibifuni kupitia kwa kifo cha ukom‐ bozi cha Kristo wako, yakomboe mawazo yetu kutokana na ufu wa tama kwa kuanzilisha mawazo ya ndani kama mlinzi juu yetu. Jicho na likaelekezwe mbali na mabaya, kusikia nako nkusielekee maneno mapotovu, na ulimi utakaswe kutokana na usemi usio‐ faa. Vitakase vinywa vyetu viimbavyo sifa zako, Ee Mungu na uizuiye mikono yetu kutenda maovu na kutenda yanayokufurahisha, ukilinda kwa nema yako viungo vyetu vyote na kuelewa kwetu.
Great and praiseworthy God, who brought us over from destruction to incorruption by the life-giving death of Your Christ, we pray You set reason within us to be the good commander over all our senses, and release them from the palsy caused by the passions. Let eyesight eschew all wicked looks, hearing be impervious to idle talk, and tongues be purged of offensive words. With Your grace, O Lord, protect our limbs and minds. Purify our lips that praise You. Make our hands abstain from evil deeds and only do what pleases You.
KASISI
PRIEST
Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.
For to You belong all glory, honor, and worship, to the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
SHEMASI
DEACON
Tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.
Again and again in peace let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako. Hekima.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace. Wisdom.
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI LA PILI LA WAUMINI
SECOND PRAYER FOR THE FAITHFUL
Ee Bwana, mtakatifu na mwema sana, tunakuomba uliye na wingi wa huruma, uturehemu sisi watenda dhambi, na utustahilishe kumpoke mwanao wa pekee Mungu wetu na mfalme wa utukufu. Kwa kuwa tazama mwili wake mtakatifu kamili na damu yake yenye thamani ikiingia kwa wakati huu, inakaribia kuwekwa kwa haya madha‐ bahu matakatifu,, akifuatwa na majeshi ya malaika kwa kutoonekana. Utujalie sisi ili bila hukumutuwe washirika wake, ili macho ya ufahamu wetu, yakian‐ gazwa kwayo, tuwe wana wa nuru na wa mchana.
Holy Master, exceedingly good, we implore You who are rich in mercy, to be merciful toward us sinners, and to make us worthy to receive Your only-begotten Son and our God, the King of glory. For His immaculate body and life-giving blood, invisibly escorted by a multitude of heavenly hosts, will now be brought in and placed on this mystical Table. Grant us to partake of them blamelessly, so that we may be illumined by them may become children of light and of the day.
KASISI
PRIEST
Kwa kadhiri ya kipawa cha neema cha Kristo Pamoja nawe umehimidiwa na Roho wako mtakatifu kamili mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote hata milele na milele.
In accordance with the gift of Your Christ, with whom and Your all-holy, good, and life-creating Spirit You are blessed, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
SHEMASI
DEACON
Enyi wakatekumeno ombeni kwa Bwana.
Catechumens, pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Hata sisi tulioamini tuombe Bwana kwa ajili ya wakatekumeno.
Let us, the faithful, pray for the catechumens.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ili awahurumie.
That the Lord have mercy on them.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Awafahamishe neno la ukweli.
That He teach them the word of truth.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Awafunulie Evangelio ya haki.
That He reveal to them the gospel of righteousness.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Awaunganishe kwa Kanisa lake moja takatifu Katholiki na la kimitume.
That He unite them to His holy, catholic, and apostolic Church.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Uwaokoe, uwahurumie, uwahifadhi, uwalinde Ee Mungu kwa neema yako.
Save them, have mercy on them, help them, and protect them, O God, by Your grace.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Enyi wakatekumeno inamisheni vichwa vyenu kwa Bwana.
Catechumens, bow your heads to the Lord.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI LA WAKATEKUMENO
PRAYER FOR CATECHUMENS
Ewe Bwana na Mungu wetu, mwumba wa viumbe vyote, unayependa watu wote kuona wokovu na kupata kujua maarifa ya ukweli wako, waangalie watumwa wako wakatikumeno na uwaokoe na dhambi zao za asili na hila za uadui; waite uzimani kwa kuangazia nafsi na miili yao na uwahesabie pamoja na kundi lako la kweli ambalo kwalo jina lako takatifu hutajwa.
God, our God, creator and maker of all, as You will that everyone be saved and come to the knowledge of the truth, look upon your servants, the catechumens, and rescue them from the ancient error and from the devil''s devices. Invite them to eternal life; illumine their souls and bodies; and include them in Your rational flock, over which Your holy name has been invoked.
KASISI
PRIEST (aloud)
Ili hawa pia pamoja nasi walitukuze jina lako adhimu na linaloheshimiwa ajabu, la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.
So that with us they also may glorify Your most honorable and majestic name, of the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
SHEMASI
DEACON
Wakatikumeno tokeni, enyi wakatikumeno tokeni. Mnaojitayarisha ubatizo mje. Mnaojitayarisha kuangazwa ombeni. Tumwombe Bwana.
All catechumens, depart; catechumens depart. All who are nearing illumination, come forward. Pray, all of you who are nearing illumination.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya ndugu zetu wote wanajitayarisha kupata Nuru takatifu na wokovu wao, sisi tulioamini tumwombe Bwana.
Let us the faithful pray to the Lord for our brethren who are nearing holy illumination and for their salvation.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ili Mungu awaanzilishe na kuwapa nguvu, tumwombe Bwana.
That the Lord our God establish and strengthen them.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ili awaangazie nuru ya hekima na uchaji Mungu, tumwombe Bwana.
That He illumine them with the light of knowledge and piety.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ili awajalie wao kwa wakati wake, kuoshwa upya kwa maondoleo ya dhambi na vazi lisiloharibika, tumwombe Bwana.
That He make them worthy in due time of the baptism of regeneration, the remissions of sins, and the robe of incorruption.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ili awafanye upya kwa maji na roho Mtakatifu, tumwombe Bwana.
That He regenerate them with water and the Spirit.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ili awajalie ukamilifu wa imani, tumwombe Bwana.
That He grant them the perfection of faith.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ili awahesabie kwa kundi lake takatifu alilochagua, tumwombe Bwana.
That He number them among His holy and chosen flock.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Uwaokoe, uwahurumie, uwahifadhi, uwalinde Ee Mungu kwa neema yako.
Save them, have mercy on them, help them, and protect them, O God, by Your grace.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ninyi mnaotarajia kuangazwa inamisheni vichwa vyenu kwa Bwana.
All who are nearing illumination, bow Your heads to the Lord.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI KWA WAJIANDAAO KUANGAZIWA
PRAYER FOR THOSE NEARING ILLUMINATION
Ee Bwana kwao hawa wanaotazamia kung’arishwa na Mwanga wa ukweli na wanaoazimia kuuvurusha uchafu wa dhambi, Angaza fikria zao. Uwaimarishe katika imani, watie nguvu kwa tumaini, uwakamilishe katika upendo; wafanye washirika wakamilifu wa Kristo uliyejitoa mwenyewe kwa ajili ya ukombozi wa wote
Master, make Your face to shine on those who are preparing for holy illumination and who long to rid themselves of sin''s contamination. Illumine their minds. Assure them in faith. Confirm them in hope. Perfect them in love. Make them precious members of Christ, who gave himself as a ransom for our souls.
KASISI
PRIEST
For You are our illumination and we offer up glory to You, the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
SHEMASI
DEACON
Ninyi mnaotarajia kuangazwa, tokeni; enyi mtarajiao kuangazwa tokeni.
All who are nearing illumination, depart. You who are nearing illumination, depart.
Wakatekumeno wote, tokeni; mkatikumeno asibaki.
All catechumens, depart. Let no catechumen remain.
LITANIES FOR THE FAITHFUL
SHEMASI
DEACON
Walioamini, tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.
All the faithful, again and again in peace let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako. Hekima.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace. Wisdom.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI LA KWANZA LA WAUMINI
FIRST PRAYER FOR THE FAITHFUL
Ee Mungu mkuu na unayesifiwa, uliyetuleta kwenye ukamilifu kutika uharibifuni kupitia kwa kifo cha ukom‐ bozi cha Kristo wako, yakomboe mawazo yetu kutokana na ufu wa tama kwa kuanzilisha mawazo ya ndani kama mlinzi juu yetu. Jicho na likaelekezwe mbali na mabaya, kusikia nako nkusielekee maneno mapotovu, na ulimi utakaswe kutokana na usemi usio‐ faa. Vitakase vinywa vyetu viimbavyo sifa zako, Ee Mungu na uizuiye mikono yetu kutenda maovu na kutenda yanayokufurahisha, ukilinda kwa nema yako viungo vyetu vyote na kuelewa kwetu.
Great and praiseworthy God, who brought us over from destruction to incorruption by the life-giving death of Your Christ, we pray You set reason within us to be the good commander over all our senses, and release them from the palsy caused by the passions. Let eyesight eschew all wicked looks, hearing be impervious to idle talk, and tongues be purged of offensive words. With Your grace, O Lord, protect our limbs and minds. Purify our lips that praise You. Make our hands abstain from evil deeds and only do what pleases You.
KASISI
PRIEST
Kwa kuwa utukufu wote na heshima na usujudu ni haki yako, ya Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote, hata milele na milele.
For to You belong all glory, honor, and worship, to the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
SHEMASI
DEACON
Tena na tena kwa amani, tumwombe Bwana.
Again and again in peace let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako. Hekima.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace. Wisdom.
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI LA PILI LA WAUMINI
SECOND PRAYER FOR THE FAITHFUL
Ee Bwana, mtakatifu na mwema sana, tunakuomba uliye na wingi wa huruma, uturehemu sisi watenda dhambi, na utustahilishe kumpoke mwanao wa pekee Mungu wetu na mfalme wa utukufu. Kwa kuwa tazama mwili wake mtakatifu kamili na damu yake yenye thamani ikiingia kwa wakati huu, inakaribia kuwekwa kwa haya madha‐ bahu matakatifu,, akifuatwa na majeshi ya malaika kwa kutoonekana. Utujalie sisi ili bila hukumutuwe washirika wake, ili macho ya ufahamu wetu, yakian‐ gazwa kwayo, tuwe wana wa nuru na wa mchana.
Holy Master, exceedingly good, we implore You who are rich in mercy, to be merciful toward us sinners, and to make us worthy to receive Your only-begotten Son and our God, the King of glory. For His immaculate body and life-giving blood, invisibly escorted by a multitude of heavenly hosts, will now be brought in and placed on this mystical Table. Grant us to partake of them blamelessly, so that we may be illumined by them may become children of light and of the day.
KASISI
PRIEST
Kwa kadhiri ya kipawa cha neema cha Kristo Pamoja nawe umehimidiwa na Roho wako mtakatifu kamili mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote hata milele na milele.
In accordance with the gift of Your Christ, with whom and Your all-holy, good, and life-creating Spirit You are blessed, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
WATU
CHOIR
WIMBO WA WAHERUVI
ENTRANCE OF PRESANCTIFIED GIFTS
Sasa, nguvu za mbinguni pamoja nasi, kwa kutoonekana zinaabudu. Tazama kwa kuwa mfalme, mfalme wa utukufu apita, [[SWA]]
Now the powers of heaven are invisibly worshiping with us. Behold, the King of glory is entering. [GOASD]
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
Kwa maombi ya mababa wetu watakatifu, Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, utuhurumie na utuokoe.
Through the prayers of our holy fathers, Lord Jesus Christ our God, have mercy on us.
WATU
CHOIR
Ona dhabihu ya siri, timilifu inafuatana na imani na tamani! Acha tukaribie kuwa washiriki wa uhai, wa milele. Alleluia. [[SWA]]
Behold, escorted is the completed mystical sacrifice. Let us approach with faith and love, to become partakers of eternal life. Alleluia, alleluia, alleluia. [GOASD]
SHEMASI
DEACON
Tumalize maombi yetu ya jioni kwa Bwana.
Let us complete our evening prayer to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya vipaji vilivyotakasika vilivyowekwa hapa mbele, tumwombe Bwana.
For the precious Gifts here presented and presanctified, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Ili Mungu wetu mpenda wanadamu aliye vipokea katika madhabahu yake matakatifu, yaliyo ya mbinguni juu na ya kiroho, kuwa manukato ya harufu ya kiroho, aturudishie neema ya Mungu, na karama ya Roho Mtakatifu, tumwombe Bwana.
That our benevolent God, having accepted them at His holy and celestial and mystical altar as an offering of spiritual fragrance, may in return send down upon us the divine grace and the gift of the Holy Spirit, let us pray.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Kwa ajili ya kuokolewa kwa kila sitikiko, ghadhabu, hatari na uhitaji, tumwombe Bwana.
For our deliverance from all affliction, wrath, danger, and distress, let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Jioni hii yote iwe kamili, takatifu, tulivu na bila dhambi, tuombe kwa Bwana.
That the whole evening may be perfect, holy, peaceful, and sinless, let us ask the Lord.
( Kidhi, Ee Bwana. )
( Grant this, O Lord. )
Kwa ajili ya kuwa na Malaika wa amani, mwongozi mwaminifu, mlinzi wa roho zetu na miili yetu, tuombe kwa Bwana.
For an angel of peace, a faithful guide, a guardian of our souls and bodies, let us ask the Lord.
Kwa ajili ya msamaha na maondoleo ya dhambi zetu na makosa yetu, tuombe kwa Bwana.
For pardon and remission of our sins and transgressions, let us ask the Lord.
Kwa ajili ya vitu vyema vifaavyo kwa roho zetu na amani ya dunia yote, tuombe kwa Bwana.
For that which is good and beneficial for our souls, and for peace for the world, let us ask the Lord.
Kwa ajili ya kumaliza maisha yetu yanayobaki kwa amani na toba, tuombe kwa Bwana.
That we may complete the remaining time of our life in peace and repentance, let us ask the Lord.
Tuombe ili mwisho wa maisha yetu uwe wa kikristo kwa amani, bila maumivu, aibu, tena tuone teto njema mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo.
And let us ask for a Christian end to our life, peaceful, without shame and suffering, and for a good defense before the awesome judgment seat of Christ.
Tukiomba umoja wa imani na ushirika wa Roho Mtakatifu, sisi na kila mmoja wetu, na wenzetu wote hata maisha yetu, kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.
Having asked for the unity of the faith and for the communion of the Holy Spirit, let us commend ourselves and one another and our whole life to Christ our God.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
Ee Mungu, mwenye mfumbo yasio elezeka, wewe uliye na hazina zote za hekima na maarifa zilizositirika, uliye tufunulia huduma ya ushirika huu, na kwa kupenda wanadamu wako umetu‐ chagua sisi wenye dhambi kukutolea vipaji na karama hizi kwa ajili ya dhambi zetu na makosa ya watu wako. Ewe mfalme usiyeonekana, unayetimiza mambo ma‐ kuu yasiyo onewa hatia, mtukufu wa ajabu uliona engi yasiyohesabika; utuangalie sisi watumwa wako wasio‐ stahili, tunaoadhimisha mbele ya madhabahu yako ma‐ takatifu kama vile mbele ya kiti chako cha rehema kati‐ kati ya wao waheruvi, ambapo mwanao wa pekee Yesu Kristo na Mungu wetu hukaa, na katika fumbo hili lililo‐ hapa madhabahuni; utuokoe sisi sote na watu wako waaminifu kutoka kwa uchafu wao wote, takasa miili na roho zetu na utakaso wako ambao hutolewi na mtu yeyote, ili tushiriki bila hukumu kwa dhamira safi, nyuso zetu bila kuona haya, mwoyo ung’aao na tuhi‐ mizwe, tuweze kuungana na Kristo mwenyewe na Mungu wetu wa ukweli aliyesema: Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, hukaa ndani yake, name kwenu na kati yetu, tuwe hekalu la Roho wako mta‐ katifu anayesujudiwa Ee Bwana uliye hai. Utukomboe na kila mitego ya Yule mwovu. Unaojitambulisha katika maneno, matendo au mafikira yetu maovu ili tuzipokee Baraka zako ulizotuagiza na watakatifu wako walioku‐ pendeza, Ee Bwana tangu milele machoni pako.
God of ineffable and unseeable mysteries, with You are the concealed treasures of wisdom and knowledge. To us You revealed the ministry of this liturgy, and in Your great love for humankind You ordained us sinners to offer You gifts and sacrifices for our misdeeds and those committed in ignorance by the people. O invisible King who do great and incomprehensible wonders, glorious, extraordinary and without number, look upon us Your unworthy servants who are standing at this Your holy Altar of sacrifice, as if it were Your cherubic throne, and on which Your only-begotten Son and our God rests through the awesome sacrament presented here; and free us and Your faithful people from every impurity, and sanctify the souls and bodies of us all with indelible sanctification, so that we may partake of this divine sacrament with a clear conscience, face unashamed, and illumined heart, and thus be enlivened by it and united to Your Christ, our true God, who said, “Those who eat my flesh and drink my blood abide in me, and I in them.” With Your Logos abiding in us and walking with us, O Lord, may we be rescued from all the wiles of the devil affecting deeds, words, or thoughts, and become temples of Your all-holy and worshipful Spirit, and thus obtain the blessings You promised us and all Your saints, who from from the beginning of time have pleased You.
KASISI
PRIEST
Na utustahilishe, Ee Bwana wa Mabwana, tukiwa na uthabiti, bila hukumu, tuwe na ujasiri kukuita Baba, wewe Mungu uliye mbinguni, na kusema:
And grant us, Master, with boldness and without condemnation, to dare call You, the heavenly God, Father, and to say:
WATU
PEOPLE
SALA LA BWANA
THE LORD’S PRAYER
Baba yetu uliye Mbinguni; Jina lako litukuzwe; Ufalme wako uje; mapenzi yako yatimizwe, hapa Duniani kama huko Mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku; na utusamehe deni zetu; kama sisi tuwasamehevyo wadeni wetu; tena usitutie majaribuni, lakini tuokoe na yule mwovu.
Our Father, who art in heaven, hallowed be Thy name. Thy kingdom come, Thy will be done, on earth as it is in heaven. Give us this day our daily bread; and forgive us our trespasses, as we forgive those who trespass against us. And lead us not into temptation, but deliver us from evil.
KASISI
PRIEST
Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, wa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.
For Thine is the kingdom and the power and the glory, of the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
KASISI
PRIEST
Amani kwa wote.
Peace be with all.
( Na iwe kwa roho yako. )
( And with your spirit. )
SHEMASI
DEACON
Tuinamishe vichwa vyetu kwa Bwana.
Let us bow our heads to the Lord.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
Ee Mungu wewe pekee mwema na mwenye huruma nyingi; unayekaa juu na kuwatazama wanyenyekevu, waangalie na uwahifadhi hawa watu wako kwa wema wa upendo wako; utujalie sisi kushiriki bila hukumu hivi vipaji vitakatifu vya uhai; kwa kuwa tumeinamisha vichwa vyetu kwako tukitazamia kwa moyo wetu wote ukarimu wa huruma zako nyingi.
Only good and compassionate God, who dwell in the highest and look upon the humble, look upon all Your people with compassionate eye, and watch over them; and make us all worthy to partake of Your life-giving sacrament without condemnation. Solemnly awaiting Your abundant mercy, we bow our heads to You.
KASISI
PRIEST
Kwa neema, na rehema, na upendo wa wanadamu wa Mwana wako wa pekee, pamoja na wewe mhimidiwa, na Roho wako Mtakatifu kamili, mwema na mpaji wa uhai, sasa na siku zote, hata milele na milele.
Through the grace, compassion, and love for humankind of Your only-begotten Son, with whom You are blessed, and Your all-holy, good, and life-creating Spirit, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
Ee Bwana Yesu Kristo Mungu wetu, toka Maskani yako matakatifu na toka enzini mwako mwa utukufu wa ufalme wako, uangalie utujie na ututakase, wewe unayekaa juu pamoja na baba, tena hapa pamoja nasi bila kuonekana. Na ukubali kutushirikisha, kwa mkono wako, Mwili wako na Damu yako heshimiwa, na kwa mikono yetu kuwashirikisha washirika wote.
Hearken, O Lord Jesus Christ our God, from Your holy dwelling place and from the throne of glory of Your kingdom, and come to sanctify us, You who are enthroned with the Father on high and are present among us invisibly here. And with Your mighty hand, grant Communion of Your most pure Body and precious Blood to us, and through us to all the people.
SHEMASI
DEACON
Tusikilize.
Let us be attentive.
KASISI
PRIEST
The presanctified Holy Gifts are for the holy.
WATU
CHOIR
Mtakatifu mmoja, Bwana ni mmoja, Yesu Kristo, kwa utukufu wa Mungu Baba. Amina.
One is Holy, one is Lord, Jesus Christ, to the glory of God the Father. Amen.
WATU
CHOIR
Wimbo wa Ushirika.
Communion Hymn.
Onjeni na mwone kwa kuwa Bwana ndiye mwema, Alleluia. [[SWA]] Alleluia.
Taste and see that the Lord is good. [SAAS] Alleluia.
SHEMASI
DEACON
Kwa kumcha Mungu, kwa imani, na upendo mkaribie.
With the fear of God, faith, and love, draw near.
Mtumwa {au mjakazi} wa Mungu {jina} anapewa Mwili na Damu ya Yesu Kristo Bwana wetu, kwa maondoleo ya dhambi na uzima wa milele.
The Body and Blood of Christ, for the remission of sins and life eternal.
WATU
CHOIR
Hymns During Holy Communion
KASISI
PRIEST
Ee Mungu, waokoe watu wako na ubariki urithi wako.
Save, O God, Your people, and bless Your inheritance.
WATU
CHOIR
Baada ya Ushirika
Hymn after Communion
Mode pl. 4.
Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima; mkate wa mbinguni na kikombe cha uhai, on‐ jeni na muone, ya kuwa Bwana ndiye mwema. Aleluia, Alleluia, Alleluia. [[SWA]]
I will bless the Lord at all times; His praise shall continually be in my mouth. Taste the heavenly bread and the cup of life, and see that the Lord is good. Alleluia, Alleluia, Alleluia. [GOASD]
SHEMASI (kwa mnong''ono)
DEACON (in a low voice)
Ee Padri, Paza
Exalt, Master.
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.
Be exalted, O God, above the heavens, and let Your glory be over all the earth.
Mhimidiwa ni Mungu wetu
Blessed is our God.
KASISI
PRIEST
Daima sasa na sikuzote hata milele na milele.
Always, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
SHEMASI
DEACON
Simameni wima; baada ya kushiriki Fumbo (Sakramenti) la umungu takatifu, bila doa, la milele, la mbinguni juu, la uzima na kuogopa kweli, tumshukuru Bwana.
Arise! Having partaken of the divine, holy, pure, immortal, heavenly, life-creating, and awesome Mysteries of Christ, let us worthily give thanks to the Lord.
( Utukufu kwako, Ee Bwana, utukufu kwako. )
( Glory to You, O Lord, glory to You. )
Utusaidie, utuokoe, utuhurumie, utuhifadhi, Ee Mungu, kwa neema yako.
Help us, save us, have mercy on us, and protect us, O God, by Your grace.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
Tukimaliza kuomba siku hii iwe kamili, takatifu, tulivu bila dhambi, sisi na kila mmoja mwenyewe na wenzetu wote, hata maisha yetu kujiweka mikononi mwa Kristo Mungu.
Having prayed for a perfect, holy, peaceful, and sinless evening, and let us commend ourselves and one another and our whole life to Christ our God.
( Kwako, Ee Bwana. )
( To You, O Lord. )
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
OMBI BAADA YA USHIRIKA MTAKATIFU
PRAYER AFTER EVERYONE COMMUNES
Tunakushukuru, Ee Mungu na Mwokozi wa watu wote, kwa baraka zako ulizoweka kwetu sisi, na kuwa umetu‐ shirikisha kwa mwili na damu yako takatifu Ee Kristo. Tena tunakuomba, Bwana mpenda wanadamu; utuhifadhi, chini ya uvuli wa mbawa zako, na utujalie hadi mwisho wa pumzi yetu kushiriki tukiwa na ustahilifu vitu vyako vitakatifu, utuangazie roho na miili yetu tuupokee urithi wa ufalme wako wa mbinguni.
We thank You, God the Savior of all, for all the blessings you have given us, and for communion of the holy body and blood of Your Christ. Benevolent Master, we pray to You: Guard us under the shelter of Your wings, and grant us till our final breath to worthily partake of Your holy sacraments, for illumination of soul and body and inheritance of the kingdom of heaven.
KASISI
PRIEST
Kwa kuwa wewe ni utakaso wetu na kwako tunatoa utukufu, kwa Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, sasa na sikuzote, hata milele na milele.
For You are our sanctification, and to You we offer up glory, to the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
KASISI
PRIEST
Twende kwa amani.
Let us go forth in peace.
SHEMASI
DEACON
Tumwombe Bwana.
Let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
KASISI
PRIEST
Ewe Bwana mwenye uwezo, uliye umba vitu vyote kwa hekima, wewe ambaye kwa maongozo yako yasiyoelezeka na upendo wako mkubwa, umetujalia siku hizi takatifu kwa ajili ya utakaso wa miili na roho zetu, ili kizingiti tamaa, na kuwa na matumaini ya ufufuo; wewe Bwana uliyempa mtumishi wako Musa mawe yaliyoandikwa na Mungu kwa Muda wa siku arobaini kwa Amri takatifu kumi. tuwezeshe nasi pia, ewe mwema, kupi‐ gana vita vyema, kumaliza mwenendo huu wa kufunga vyema, kuweka imani bila kugawanyika, kuseta vichwa vya nyoka wasioonekana, kuwa na ushindi juu ya dhambi, na kuambudu ufufuo mtakatifu bila hukumu. Kwa kuwa kubarikiwa na kutukuzwa ni kwa jina lako adhimu na linalo‐ heshimiwa la baba na Mwana na Roho Mtakatifu, sasa na siku zote hata milele na milele.
Master and Ruler over all, You made all creation in wisdom. By Your ineffable providence and abounding goodness You brought us to these solemn days, for cleansing of soul and body, self-control over passions, and hope of resurrection. Good Lord, who for Moses Your servant forged the divinely engraved tablets in the course of forty days, to us also grant to fight the good fight, to finish the race of the fast, to keep the faith intact, to shatter the heads of invisible dragons, to emerge as victors over sin, and to be ready without condemnation to venerate Your holy resurrection.
For blessed and glorified is Your all-honored and majestic name, of the Father and the Son and the Holy Spirit, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
WATU
CHOIR
Jina la Bwana, lihimidiwe, tangu sasa hata milele (3)
Blessed be the name of the Lord, from this time forth and to the ages. (3)
KASISI (kwa mnong''ono)
PRIEST (in a low voice)
Ewe Bwana Mungu wetu, uliye tu‐ wezesha kunyenyekea siku hizi za kufunga, na uliye tujalia kushiriki fumbo lako lisiloelezeka kuogofya, tuunganishe na kundi lako la kweli na tuwe warithi wa ufalme wako, sasa na siku zote, hata milele na milele. Amina.
Lord our God, You brought us to these solemn days and made us partakers of Your awesome sacraments, unite us to Your rational flock, and make us heirs of Your kingdom, now and ever and to the ages of ages. Amen.
SHEMASI
DEACON
Tumwombe Bwana.
Let us pray to the Lord.
( Bwana, hurumia. )
( Lord, have mercy. )
KASISI
PRIEST
Baraka ya Bwana na huruma yake imfikie ninyi, kwa neema yake ya Umungu na upendo wake kwa wanadamu, daima, sasa na siku zote hata milele na milele.
May the blessing and the mercy of the Lord come upon you by His divine grace and love for humankind, always, now and ever and to the ages of ages.
( Amina. )
( Amen. )
Utukufu kwako, Ee Kristo Mungu wetu na matumaini yetu, utukufu kwako.
Glory to You, O Christ God, our hope. Glory to You.
Yeye Kristo Mungu wetu wa kweli, kwa maombi ya Mama yake asiye na doa na asiye na waa, mtakatifu kamili; kwa nguvu ya msalaba wenye thamani na mpaji wa uhai; kwa ulinzi wa nguvu zisizo na mwili waheshimiwa wa mbinguni; kwa maombi ya Yohana, Nabii, mtangulizi na mbatizaji, mheshimiwa na wa sifa; ya Mitume watakatifu, watukufu na wasifiwa; ya mashahidi watakatifu, wasifiwa na washindaji wazuri; ya watawa watakatifu na wacha Mungu; (Mtakatifu wa Kanisa); ya watakatifu na wenye haki Yohakim na Anna; na ya watakatifu wote, atuhurumie na atuokoe, yu Mungu mwema, mrahimu na mpenda wanadamu.
May Christ our true God, through the intercessions of His all-pure and all-immaculate holy Mother, the power of the precious and life-giving Cross, the protection of the honorable, bodiless powers of heaven, the supplications of the honorable, glorious prophet and forerunner John the Baptist, of the holy, glorious, and praiseworthy apostles, of the holy, glorious, and triumphant martyrs, of our righteous and God-bearing fathers, (local patron saint); of the holy and righteous ancestors of God Joachim and Anna, and of all the saints, have mercy on us and save us, as He is good, benevolent, and merciful God.
MSOMAJI
READER
Zaburi ya 33 (34).
Psalm 33 (34).
Nitamhimidi BWANA kila wakati, sifa zake zi kinywani mwangu daima.
I will bless the Lord at all times; His praise shall continually be in my mouth.
Katika BWANA nafsi yangu itajisifu, wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
My soul shall be praised in the Lord; let the gentle hear, and be glad.
Mtukuzeni BWANA pamoja nami, na tuliadhimishe jina lake pamoja.
Oh, magnify the Lord with me, and let us exalt His name together.
Nalimtafuta BWANA akanijibu, akaniponya na hofu zangu zote.
I sought the Lord, and He heard me; and He delivered me from all my sojourning.
Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, wala nyuso zao hazitaona haya.
Come to Him, and be enlightened, and your face shall never be ashamed.
Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, akamwokoa na taabu zake zote.
This poor man cried, and the Lord heard him, and saved him from all his afflictions.
Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
The Angel of the Lord shall encamp around those who fear Him, and He will deliver them.
Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; heri mtu yule anayemtumaini.
Oh, taste and see that the Lord is good; blessed is the man who hopes in Him.
Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, yaani, wamchao hawahitaji kitu.
Fear the Lord, you His saints, for there is no want for those who fear Him.
Wana-simba hutindikiwa, huona njaa; bali wamtafutao BWANA hawahitaji kitu chochote kilicho chema.
Rich men turned poor and went hungry; but those who seek the Lord shall not lack any good thing.
Njoni, enyi wana, mnisikilize, nami nitawafundisha kumcha BWANA.
Come, you children, listen to me; I will teach you the fear of the Lord.
Ni nani mtu yule apendezwaye na uzima, apendaye siku nyingi apate kuona mema?
Who is the man who desires life, who loves to see good days?
Uuzuie ulimi wako na mabaya, na midomo yako na kusema hila.
Keep your tongue from evil, and your lips from speaking deceit.
Uache mabaya ukatende mema, utafute amani ukaifuatie.
Shun evil and do good; seek peace and pursue it.
Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, na masikio yake hukielekea kilio chao.
The eyes of the Lord are upon the righteous, and His ears are open to their supplications.
Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya, aliondoe kumbukumbu lao duniani.
The Lord’s face is against those who do evil, so as to destroy their remembrance from the earth.
Walilia, naye BWANA akasikia, akawaponya na taabu zao zote.
The righteous cried, and the Lord heard them; and He delivered them from all their afflictions.
BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo, na waliopondeka roho huwaokoa.
The Lord is near those who are brokenhearted, and He will save the humble in spirit.
Mateso ya mwenye haki ni mengi, lakini BWANA humponya nayo yote.
Many are the afflictions of the righteous, but He will deliver them from them all.
Huihifadhi mifupa yake yote, haukuvunjika hata mmoja.
The Lord shall guard all their bones; not one of them shall be broken.
Uovu utamwua asiye haki, nao wamchukiao mwenye haki watahukumiwa.
The death of sinners is evil, and those who hate the righteous shall go wrong.
BWANA huzikomboa nafsi za watumishi wake, wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao. [[SWA]]
The Lord will redeem the souls of His servants, and all who hope in Him shall not go wrong. [SAAS]
Zaburi ya 144 (145).
Psalm 144 (145)
Ee Mungu wangu, mfalme, nitakutukuza, nitalihimidi jina lako milele na milele.
I shall exalt You, my God and my King, and I shall bless Your name forever and unto ages of ages.
Kila siku nitakuhidi, nitalisifu jina lako milele hata milele na milele.
Every day I shall bless you and praise Your name forever and unto ages of ages.
BWANA ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, wala ukuu wake hautambulikani.
Great is the Lord and exceedingly praiseworthy, and His greatness has no limit.
Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, kitayatangaza matendo yako makuu.
Generation and generation shall praise Your works, and they shall declare Your power.
Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, na matendo yako yote ya ajabu.